Monday, 9 June 2014

Seedorf afukuzwa AC Milan,Inzaghi kocha mkuu

Inzaghi na Seedorf enzi zao dimbani
Klabu ya AC Milan ya Italia imeamua kumtimua kocha wake Clarence Seedorf na kumuajiri Filippo Inzaghi kuchukua nafasi hiyo.
Seedorf raia wa Uholanzi aliteuliwa kuinoa timu hiyo Januari mwaka huu kuchukua nafasi ya Massimiliano Allegri aliyetimuliwa.
Pamoja na kuingoza timu hiyo kukaribia kupata nafasi ya kucheza michuano ya Europa League, ilitegemewa Seedorf kuachia manyanga kutokana na kushindwa kuelewana na rais Silvio Berlusconi pamoja na ofisa mkuu Adriano Galliani.
Klabu hiyo sasa imethibitisha kumtimua kiungo huyo wa zamani wa timu hiyo na kumchagua Inzaghi kuziba nafasi yake baada ya kuingoza vyema timu ya vijana chini ya umri wa miaka 19 aliyokuwa akiifundisha.

0 comments:

Post a Comment