Monday, 9 June 2014

Jiji la Sao Paulo lachafuka kwa fujo,siku tatu zimebaki kuelekea kombe la dunia

Polisi nchini Brazil wamelazimika kutumia mabomu ya machozi dhidi ya waandamanaji katika jiji la Sao Paulo ikiwa ni siku tatu kabla ya michuano ya Kombe la Dunia haijaanza kutimua vumbi mchezo wa ufunguzi katika mji huo.
Taarifa zinaeleza  kuwa zaidi ya waandamanaji 300 walikuwepo mtaani na helikopta zilikuwa zikizunguka juu yao. Waandamanaji hao waliitwa na wafanyakazi wa Sao Paulo ambao waligoma kuunga mkono ongezeko la asilimia 12.2 la mshahara.
Rais wa Brazil Dilma Rousseff amesema hataruhusu vurugu ya vurugu kuingilia michuano ya Kombe la Dunia.

0 comments:

Post a Comment