Taifa Stars yaichomoa Zimbabwe,sasa kucheza na Msumbiji
Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) imefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa Afrika AFCON mara baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Zimbabwe au Mighty Warios Ugenini.
Magoli ya Stars yalifungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ pamoja na Thomas Ulimwengu huku yale ya wenyeji yakifungwa na Danny Phiri na Willard Katsande.
Matokeo hayo ya sare
yanaifanya Stars kuibuka na ushindi wa jumla yamabao 3-2 kufuatia
kushinda goli 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Jijini Dar es Salam.
Kufuatia kufanikiwa kupita mbele ya Zimbabwe sasa Taifa Stars watapaswa kuendelea na maandalizi mazuri ili kuweza kuwakabili vilivyo Msumbiji.
Kufuatia kufanikiwa kupita mbele ya Zimbabwe sasa Taifa Stars watapaswa kuendelea na maandalizi mazuri ili kuweza kuwakabili vilivyo Msumbiji.
0 comments:
Post a Comment