Monday, 23 June 2014

Yanga yasajili wawili,Barthez aongezewa mkataba.

YANGA SC imekamilisha usajili wa wachezaji wawili wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi Mart Nooij
Habari kutoka Yanga ni kwamba wachezaji waliosajiliwa ni beki Pato Ngonyani na kiungo mkabaji, Said Juma.
Aidha, Yanga SC pia imesajili mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Saleh Abdallah. Ngonyani anayecheza kushoto na nafasi zote za kati, amesaini Mkataba wa miaka mitatu, wakati Said Juma amesaini miaka miwili na Saleh Abdallah amesaini miaka mitatu pia.
Aidha, Yanga SC imewaongezea mikataba wachezaji wake Jerry Tegete, Said Bahanuzi, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Ally Mustafa ‘Barthez’ ambao wote wamesaini miaka miwili kila mmoja.
Yanga SC imesitisha mpango wa kumtema kiungo Nizar Khalfan ambaye amebakiza mwaka mmoja, wakati kipa kipa Yusuph Abdul, mabeki David Luhende, Ibrahim Job, viungo Athuman Idd 'Chuji', Geroge Banda, Rehani Kibingu, Hamisi Thabiti, Bakari Masoud, Abdalllah Mguhi ‘Messi’ na washambuliaji Reliants Lusajo na Shaaban Kondo wameachwa.
Yanga SC sasa imekamilisha usajili wa wachezaji wa ndani na sasa inataka kuongeza mchezaji mmoja wa kigeni.
Simba SC ilikuwa ina mpango wa kumrudisha kipa wake Ally Mustafa ‘Barthez’ na kwa kuongeza mkataba Jangwani, maana yake Wekundu wa Msimbazi;
Chanzo;Binzubeiry

0 comments:

Post a Comment