Breaking News; Mario Mandzukic Asaini miaka minne Athletico Madrid.
Mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic amesaini mkataba wa miaka minne wa kuichezea klabu ya Atletico Madrid akitokea Bayern Munich, klabu hiyo inayoshiriki La Liga imetangaza hii leo.Mabingwa hao wa Hispania wamekubali kumchukua mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 ili kuziba nafasi ya Diego Costa aliyejiunga na Chelsea.
Mandzukic amechukua uamuzi huo baada ya kutua kwa Robert Lewandowski aliyekuwa anaitumikia Borussia Dortmund.
" Ujio wa Mario Mandzukic ni habari njema kwetu kwani ni mchezaji anayefaa kwenye nafasi hi.,"alisema mkurugenzi wa Atletico Jose Luis Perez Caminero kupitia mtandao wa klabu (www.clubatleticodemadrid.com).
Mandzukic ameitumikia Munich kwa miaka miwili na kufunga mabao 33 katika michezo 54 ya Bundesliga Alifunga bao la kuongoza dhidi ya Dortmund katika fainali ya ligi mwaka 2013 , ambapo Bayern walishinda 2-1.
Mshambuliaji huyo amefunga mabao 15 katika michezo 52 kwa upande wa Croatia, yakiwamo yale mawili katika fainali za kombe la dunia mwaka huu Kule Brazil.
Atletico walitwaa ubingwa wa La Ligabaada ya miaka 18 na kutinga fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment