Evra kutua Juventus,Loris aongeza miaka mitano Spurs.
Mchezaji wa Manchester United Patrice Evra anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa €3.5 million ili kujiunga na Juventus baada ya kukubali mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo.Raia huyo wa Ufaransa alisaini mkataba mwingine wa mwaka moja ndani ya klabu ya Man United mwezi May lakini baada ya kutua kwa Luke Shaw kwa kiasi cha €38 million nafasi yake imekuwa ngumu.
Naye kipa wa kimataifa wa Ufaransa, Hugo Lloris amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu ya Tottenham Hotspurs.
Lloris mwenye umri wa miaka 27 alisajiliwa na meneja wa zamani wa Spurs Andre Villas-Boas kwa paundi milioni nane akitokea Olympique Lyon katika kipindi cha usajili mwaka 2012.
Golikipa huyo ambaye ameichezea Spurs mechi 78 ndiye alikuwa nahodha wa Ufaransa katika michuano ya Kombe la Dunia huku akicheza mechi zote sita za nchi hiyo kwenye michuano hiyo inayoendelea nchini Brazil.
Lloris atafanya kazi na kocha wa tatu toka ajiunge na Spurs ambapo Mauricio Pochettino atachukua mikoba ya Tim Sherwood aliyetimuliwa baada ya kumalizika kwa msimu wa 2013-2014.
0 comments:
Post a Comment