Breaking News;Manchester United hoi kwa Kroos,asaini miaka sita Madrid.
Kiungo wa Ujerumani Toni Kroos amesaini mkataba wa miaka sita wa kuitumikia klabu ya Real Madrid akitokea Bayern Munich,imethibitisha klabu ya Munich.Mchezaji huyo mwenye miaka 24 alikuwa mchezaji imara ambaye aliipa ubingwa wa kombe la dunia Ujerumani dhidi ya Argentina katika mchezo wa fainali huku Ujerumani ikishinda 1-0.
Kroos amejiunga na wababe hao wa Bernabeu kwa uhamisho wa kiasi cha euro mili 25 sawa na ($33.82 million).
Kroos alikuwa chaguo la kwanza ndani ya Madrid kwenda kurithi kazi ya Xabi Alonso. Ujio wake unasukuma zaidi kwa Sami Khedira kujiunga na vilabu vya Uingereza
"Tunamshukuru sana Toni Kroos kwa kuitumikia Munich," alisema mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenig.
Manchester United ilionesha nia ya kumsajili lakini Kroos mwenyewe alichagua kwenda Madrid.
Kroos alijiunga na klabu ya vijana ya Bayern 2006 akiwa na miaka 16. Amecheza michezo 170 ndani ya Bayern baada ya kupandishwa timu ya wakubwa 2007 lakini baadaye alipelekwa kwa mkopo Bayer Leverkusen kuanzia 2009 hadi mwaka 2010.
0 comments:
Post a Comment