Thursday, 17 July 2014

Mgimwa ameanza vita na Tambwe.

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba Michael Mgimwa, amepania kumpiku Amis Tambwe katika ufungaji wa mabao wakati msimu mpya utakapoanza Sepemba 20.
Mgimwa aliyejiunga saini mkataba wa miaka miwili Simba akitokea timu ya Roi Et United ya Thailand amesema kuwa atahakikisha hilo linawezekana kutokana na uzoefu wa miaka miwili alioupata akiwa huko.
“Najisikia mwenye fuaha kucheza Simba kwa sababu ni timu kubwa hapa Tanzania kikubwa nataka kuwamfungaji bora katika msimu wangu wa kwanza ili kupambana na Tambwe lengo ni kuhakikisha Simba inakuwa bingwa mwishoni mwa msimu,”alisema Mgimwa.
Mgimwa raia wa Tanzaniza kabla hajakwenda Thailand aliwahi kuichezea timu ya vijana ya Mtibwa Sugar na baadaye alipitia kituo cha kukuza vipaji kilichokuwa kinamilikiwa na Shirikisho la soka Tanzania TFF,kikijulkana kama TSA.

0 comments:

Post a Comment