Mkongwe EL Hadary kurudi Zamalek lakini Mido amgomea.
Klabu ya Zamalek ya Misri imefikia makubaliano na golkipa mkongwe Essam El Hadary ili arudi tena kuitumikia klabu hiyo kwa msimu unaofuata..Kipa huyo mwenye miaka 41 bado ana mkataba wa miaka miwili na klabu ya Wadi Degla.
Taarifa za ndani kutoka huko Misri ambazo zimenaswa na Sports4lifetz zimeeleza kuwa El Hadary alikutana na mwenyekiti Mortada Mansour na kufikia makubalianao ambapo kipa amesema kuwa atavunja mkataba na klabu yake ya Degla.
Kipa wa sasa wa klabu ya Zamalek Abdel Wahed Al Sayed mapema mwaka huu alitangaza kuwa ligi ikimalizika atatangaza kustaafu soka.
Zamalek imejaribu kuongea na makipa wengi wa pale Misri lakini wamegoma kujiunga mfano kipa wa Al Ismaily Mohamed Awad na kipa wa Al Masry Ahmed El Shenaway.
El Hadary alianza kucheza akiwa na klabu ya Damietta akajiunga na Al Ahly mwaka 1996 hadi 2008 akajiunga na FC Sion hadi 2009 kabla ya kujiunga na Al Ismaily 2009 hadi 2010 halafu akajiunga na Zamalek mwaka 2010 lakini akatimkia klabu Al-Merreikh ya Sudan na 2013 akajiunga na Wadi Degla.
Lakini kocha wa Zamalek Ahmed Hossam Mido amemwambia mwenyekiti wake kuwa hataki kumwona Al Hadary katika klabu
0 comments:
Post a Comment