Monday, 21 July 2014

Gerard astaafu soka la kimataifa,Soma wasifu wake.

Kiungo wa klabu ya Liverpool na nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza  Steven Gerrard amestaafu kucheza soka la kimataifa.
Gerrard, mwenye miaka  34 aliiongoza Uingereza katika fainali za kombe la dunia mwaka huu kule Brazil ambapo Uingereza iliondolewa katika hatua ya makundi.
Kiungo huyo kwa mara ya kwanza alianza kucheza soka mwaka 2000 mchezo dhidi ya Ukraine backmwezi mei na kuichezea Uingereza michezo  114 na kufunga mabao  21.

Akizungumza kwenye tovuti ya chama cha soka cha Uingereza  FA amesema: "nimefurahia kila dakika niliyowakilisha nchi yangu na ni siku ya masikitiko kufahamu sitovaa tena jezi ya Uingereza.".
Gerard amesemabaada ya kurudi kutoka Brazil amefanya majadiliano na marafiki zake pamoja na familia yake.
 Gerard amesema ameelekeza nguvu zake katika klabu ya Liverpool na atajituma zaidi katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu.
Wasifu
Jina kamili Steven George Gerrard
Kuzaliwa 30 May 1980 (miaka 34)
Mahali alipozaliwa Whiston, Merseyside, England


Nafasi Uwanjani Kiungo
Klabu
Kwa sasa
Liverpool
Jezi namba 8
Timu ya vijana
1987–1998 Liverpool
wakubwa
Mwaka timu michezo  Mabao
1998– Liverpool 475 (111)
Timu ya taifa
1999–2000 England U21 4 (1)
2000–2014 England 114 (21)

0 comments:

Post a Comment