Monday, 21 July 2014

Rodriguez anukia Madrid,ameandaliwa paundi mil.60

Mfungaji bora wa fainali za kombe la dunia 2014 kule Brazil mcolombia James Rodriguez anakaribia kujiunga na Klabu ya Real Madrid kwa mujibu wa ripoti mbalimbali.
Gazeti la  daily mail limeripoti kuwa rais wa Real Madrid Florentino Perez ambaye alikuwa katika biashara zake Amerika ya Kusini amerejea ili kuhakikisha wanamnasa Rodriguez.
Wakati gazeti la Macca limeripoti kuwa kocha  Carlo Ancellotti amekwishaelezwa kila kitu kuhusu mchezaji huyo kujiunga na Madrid.
Uhamisho wa mshambuliaji huyo ambaye anatarajia kusaini mkataba wa miaka sita na Madrid jumatano wiki hii una thamani ya paundi milioni 60.
Madrid ikifanikiwa kumnasa Rodriguez itakuwa imetumia paundi mil 80 baada ya kumnasa mchezaji wa Bayern Munich Toni Kroos kwa paundi mil.20  juma lililopita.

0 comments:

Post a Comment