John Cena kazi anayo,kutetea ubingwa dhidi ya Kane,Randy na Reigns.
Hapo juzi (Juni 29) John Cena alitangazwa rasmi kuwa bingwa wa mieleka mwaka 2014 baada ya kuwagaragaza wanaume 7 waliokuwa ulingoni kupambana katika mchezo wa WWE Money in the Bank.Lakini hii leo tarifa zilizotolewa na uongozi wa mchezo huo kupitia kwa Triple H zimeeleza kuwa John Cena atatetea ubingwa wake dhidi ya wanamieleka watatu ambao ni Randy Orton, Kane na Roman Reigns na mchezo huo umepew jina la Fatal 4-Way.
Lakini taarifa hizo zimepingwa na wadau wa mchezo huo wakidai kuwa Triple H amettumia mabavu baada ya Cena kukata wito pale alipoitwa na uongozi wa mchezo huo na baadaye akapewa mchezo huo.
Ikumbukwe kuwa John Cena aliwashinda wanamieleka Kane,Roman Reigns, Randy Orton, Bray Wyatt, Bingwa wa Marekani Sheamus, Cesaro na Alberto Del Rio katika mchezo huo unaohusisha ngazi ili kumpata bingwa mpya wa uzito wa juu duniani.
Kwa maana hiyo John Cena atakumbana na wanaume hao na mchezo utapigwa July 20.
Hapo kabla bingwa anayemiliki mkanda huo Daniel Bryan alijitoa rasmia June 9 baada ya kutopona vema na bado hajakamilisha matibabu yake.
Katika mchezo wa juzi Orton alipigwa ngazi kichwani na kuchanika na kumfanya aumie vibaya lakini madakatari walimpa matibabu ambapo ameshonwa nyuzi kadhaa.

0 comments:
Post a Comment