Sunday, 20 July 2014

John Cena kutetea ubingwa wa mieleka leo hii.

Mwishoni mwa mwezi uliopita  (Juni 29) John Cena alitangazwa rasmi kuwa bingwa wa mieleka mwaka 2014 baada ya kuwagaragaza  wanaume 7 waliokuwa ulingoni kupambana katika mchezo wa  WWE Money in the Bank.
John Cena atapanda ulingoni leo(Julai 20) kupambana na wanaume au  wanamieleka watatu ambao ni Randy Orton, Kane na Roman Reigns na mchezo huo umepew jina la  Fatal 4-Way.
Mapema  taarifa hizo zilizotangaza na Triple H kuhusu mchezo huu zilipingwa na wadau wa mchezo huo wakidai kuwa Triple H ametumia mabavu baada ya Cena kukata wito pale alipoitwa na uongozi wa mchezo huo na baadaye akapewa mchezo huo.
Ikumbukwe kuwa John Cena aliwashinda wanamieleka Kane,Roman Reigns, Randy Orton, Bray Wyatt, Bingwa wa Marekani  Sheamus, Cesaro na  Alberto Del Rio katika mchezo huo unaohusisha ngazi ili kumpata bingwa mpya wa uzito wa juu duniani.
Hapo kabla bingwa anayemiliki mkanda huo Daniel Bryan alijitoa rasmia   baada ya  kutopona vema na bado hajakamilisha matibabu yake.
Mchezo huo utakuwa na mvuto wa aina yake kutokana na John Cena kuwa katika kiwango chake kizuri.

0 comments:

Post a Comment