Sunday, 20 July 2014

Mourinho amtetea bosi wake wa zamani Van Gaal asema ni mkweli.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kocha  mpya wa Manchester United Louis van Gaal si Mtu wa kiburi ila ni mkweli.
Mourinho  alifanya kazi chini ya Van Gaal huko Barcelona kati ya Mwaka 1997 na 2000 na kutwaa Ubingwa wa La Liga mara 2, Copa del Rey 1 na UEFA Super Cup.
Kocha huyo wa Chelsea amesema Van Gaal yuko sawa alipotamka kuwa lengo lake ni kutwaa Ubingwa na si kumaliza ndani ya 4 Bora.
Mourinho amesema: “Nimesikiliza Mahojiano yake na Wanahabari na nadhani alijionyesha yuko vilevile, Van Gaal yule yule, Mtu mkweli na mchambuzi. Ukiwa mkweli na mtu wa moja kwa moja unasema unalotaka, na hiyo haimaanishi una kiburi bali ni mkweli!”
Mourinho alifafanua: “Alisema walimaliza nje ya 4 Bora na anataka kubadilisha hilo. Ni wazi anataka kuwa Bingwa. Alichosema ni sahihi!”
Van Gaal, ambaye aliteuliwa kuwa kochaa mpya wa Man United Mwezi Mei, alijiunga kwa mara ya kwanza na Timu yake mpya Juzi Jumatano baada ya kuiongoza Uholanzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil na kuifikisha Nafasi ya Tatu.
Alhamisi, Van Gaal alitambulishwa rasmi kuwa mkufunzi mpya wa Man United huko Old Trafford na kisha kufanya Mahojiano na Wanahabari.
Hivi sasa Van Gaal na Kikosi chake wako huko Los Angeles Marekani kuwania Chevrolet Cup.
Baada ya hiyo watapambana na AS Roma, Inter Milan na Real Madrid kuwania International Champions Cup na wakifuzu kuingia Fainali watacheza Mechi yao ya 5 huko Marekani hapo Agosti 4.
Mechi ya kwanza kwa Van Gaal Uwanja wa Nyumbani Old Trafford ni dhidi ya Valencia hapo Agosti 12 na Siku 4 baadaye wataanza Msimu mpya wa Ligi Kuu Uingereza  kwa kuivaa Swansea City pia Uwanja wa Old Trafford.

0 comments:

Post a Comment