Klabu ya Manchester United itatoa kiasi cha £10 million kwa ajili ya mlinzi wa Arsenal Thomas Vermaelen.
Klabu ya Paris Saint-Germain inakaribia kumnasa mchezaji Angel Di Maria,mchezaji huyo amekubali kujiunga wakati huo Edinson Cavani anataraji kwenda Manchester United
Klabu ya Manchester United wamerudisha tena nia yao ya kumsajili mchezaji wa Paris Saint-Germain
Edinson Cavani iwapo Wayne Rooney atashindwa kumshawishi vizuri Louis van
Gaal.
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal ameandaa kiasi cha €12.5 million kwa ajili ya kumnasa mlinzi wa kati wa Feyenoord Stefan de Vrij.
Liverpool wao wameanza kumsaka mchezaji wa Man city James Milner
Everton ina imani kuwa Romelu Lukaku atajiunga nao ila Chelsea wanataka kiasi cha £20 million kwa ajili ya nyota huyo wa Ubelgiji.
Liverpool iko mbioni kumsajili kipa wa Fiorentina Neto baada ya kipa wa Swansea City Michel Vorm ugoma kujiunga nao.
0 comments:
Post a Comment