Kikosi cha ovyo kombe la dunia 2014,kinaongozwa na Casillas,usipitwe jisomee mwenyewe.
Wakati mchezo wa fainali za kombe la dunia unataraji kupigwa hii leo kati ya Ujerumani na Argentina,waandishi wa habari wa Reuters wamechagua kikosi cha ovyo cha fainali za mwaka huu (4-3-3):Sports4lifetz inakupatia kikosi hicho
Kipa: Iker Casillas (Hispania)
Walinzi: Dani Alves (Brazil), Sergio Ramos (Hispania), Pepe (Ureno), Benoit Assou-Ekotto (Cameroon)
Viungo: Eden Hazard (Ubelgiji), Shinji Kagawa (Japan), Alex Song (Cameroon)
Washambuliaji: Fred (Brazil), Mario Balotelli (Italia), Cristiano Ronaldo (Ureno
Kipa: Iker Casillas (Hispania).
Alikuwa kipa chaguo la kwanza kwa nchi yake akiwaweka benchi Pepe Reina na David de Gea ingawa alishaachwa kuwa chagua la kwanza la Real Madrid. Alifungwa goli 5-1mbele ya Uholanzi akafungwa 2-0 na Chile,aliondoka Brazil akiwa na aibu.
Beki upande wa kulia: Dani Alves (Brazil). Beki huyo wa Barcelona alipwaya sana mpaka kocha wake Luiz Felipe Scolari akaanza kumtumia mkongwe Maicon ili angalau aokoe jahazi la Brazil.ni tofauti na alivyokuwa anacheza Barcelona.
Beki wa kati: Pepe (Ureno). Beki wa Real Madrid alianza mashindano kwa fedheha baada ya kupigwa kadi nyekundu wakati Ureno ikibamizwa 4-0 na Ujerumani baada ya kuonekana kama alimpiga kichwa na kumtolea maneno machafu Thomas Mueller. Alifungiwa mchezo dhidi ya Marekani ,alirudi mchezo dhidi ya Ghana na Ureno kushinda 2-1 japo walishindwa kuingia 16.
Beki wa kati: Sergio Ramos (Hispania). Ramos alionekana angeisaidia Hispania baada ya kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa upande wa vilabu ,mchezo wa kwanza tu walibamizwa na Uholanzi 5-1 akashindwa kuonesha makali yake.
Kushoto; Benoit Assou-Ekotto (Cameroon). Alifanya kituko kibaya sana ambapo vyombo vingi vya habari viliandika sana na kuripoti na hata mtandao huu wa Sports4lifetz uliripoti baada ya kupigana na mcameruni mwenzake Benjamin Moukandjo baada ya kupigwa 4-0 na Croatia. mchezo uliofuata dhidi ya Brazil aliachwa na kocha wake.
Kiungo: Eden Hazard (Belgium). Kikosi hicho kiliitwa "golden generation", Hazard alicheza vizuri mchezo moja tu lakini michezo iliyofuata hakuonekana..
Kiungo: Shinji Kagawa (Japan). Si yule ambaye aliipa ubingwa mara mbili Borussia Dortmund katika Bundesliga , Kagawa alitolewa mchezo dhidi ya Ivory Coast na mchezo dhidi ya Ugiriki alionesha kiwango cha hali ya chini . Hakuwa Kagawa aliyezoeleka.
Kiungo: Alex Song. Baada ya mjomba wake Rigobert Song kutolewa kwa kadi nyekundu mwaka 1994 na 1998, Song aliendeleza desturi ya familia yake pale alipompiga kiwiko mcroatia Mario Mandzukic akatolewa nje wakati Croatia ilikuwa inaongoza 1-0 mwishoni Cameroon walicharazwa 4-0 na walitolewa moja kwa moja . Song, alifungiwa michezo mitatu ingawa mwishoni aliomba msamaha.
Mshambuliaji: Fred. Akina Jairzinho, Careca, Romario, Bebeto na Ronaldo hawatalinganishwa na Fred kutokana na kuonesha kiwango kibovu mno,Ferd anaondoka kwenye mashindano akiwa mshambuliaji namba 9 aliyefunga bao moja tu.
Mshambuliaji: Cristiano Ronaldo. Ingawa alikuwa anaumwa katika mashindano ya mwaka huu hakucheza kama ilivyozoeleka,hakupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wachezaji wenzake ndani ya timu ya Ureno.Ronaldo hakusaidia chochote ndani ya Ureno ingawa ndiye aliyeipeka Ureno kwenye mashindano kule Brazil mbele ya Sweden akifunga mabao yote nje ndani,mchezo dhidi ya Ghana alifunga bao.
Mshambuliaji wa katii: Mario Balotelli. Alkifunga bao la ushindi dhidi ya England, "Supermario" alishindwa kuonesha kiwango mbele ya Costa Rica na Uruguay. Alikosa nafasi nyingi tu kwa hizo timu za Amerika,alipondwa sana kule Italia kwa kushindwa kuibeba timu tofauti na enzi za akina Totti au Del Piero.
0 comments:
Post a Comment