Sunday, 13 July 2014

Tuko tayari kutengeneza historia-Ujerumani.

Kocha wa Ujerumani Joachim Loew amesema wanadhamiria kufanya historia kwa kushinda fainali ya  Kombe la Dunia mchezo utakaopigwa leo na kuwa taifa la kwanza la bara Ulaya kutwaa taji hilo huko Amnerika  Kusini.
Kikosi chake kitachuana na Argentina katika uwanja wa Maracana, Rio de Janeiro huku Loew na vijana wake wana matumaini ya kushindia taifa lao taji lake la nne.
Hakuna taifa la bara la Ulaya  limetwaa taji hilo kwenye awamu nane za shindano hilo zilizoandaliwa Amerika  Kusini lakini kocha huyo anashikilia kuwa kikosi chake kitaunda historia.
“Licha ya yale yametendeka hapo zamani, ni swala la ushindi sasa na tunafahamu tunaweza kuandika historia kwasababu timu za Marekani Kusini wameweza kuwika nyumbani.
“Itakuwa ni furaha zaidi ikiwa tutanyakua taji hili kwenye ardhi ya Amerika Kusini na sioni sababu ya kukosa uwezo,” mwalimu huyo alisema.
Itakuwa ni mara ya sita kwa Ujerumani na Argentina kukutana kwenye Kombe la Dunia na mara ya tatu kucheza katika fainali huku wahasimu hao wakitoshana 1-1 kwenye mechi za uamuzi.
Kiungo maahiri, Bastian Schweinsteiger, alichangia kuwa Ujerumani hawana shinikizo lolote.
“Kwangu, si changamoto kubwa zaidi kwani kila mechi katika awamu ya mwondoano ni changamoto kweli.
“Tumekomaa kama kikosi na tumedhihirisha ubora wetu miaka michache iliyopita na tunazidi kusonga mbele. Itakuwa masikitiko tufungwa  lakini hatutasambaratika,” mchezaji huyo aliongeza.
Mchezo huo utapigwa majira ya saa nne usiku .

0 comments:

Post a Comment