Maskini Brazil wapigwa 3-0,Uholanzi washindi wa tatu na dola millioni 18 zao.
Timu ya taifa ya Uholanzi imeshika nafasi ya tatu katika mashindano ya kombe la dunia kwa mwaka 2014 kule nchini Brazil baada ya kuwafunga wenyeji Brazil mabao 3-0 mchezo uliomalizika muda mfupi uliopita.Uholanzi ambayo ilitolewa na Argentina katika hatua ya nusu fainali ilipata mabao mawili ndani ya dakika 16.
Baada ya kukosekana katika mchezo ambao walidhalilishwa mabao 7-1 na Ujerumani beki Thiago Silva, alirudi lakini kwa bahati mbaya upande wake alimwangusha Arjen Robben katika eneo la hatari na Robin van Persie akafunga mkwaju huo wa pelnati.
![]() |
Daley Blind akishangilia bao la pili |
Kipa wa Uholanzi Jasper Cillessen alionekana kikwazo kwa Brazil hii leo na bao la tatu lilifungwa na Georginio Wijnaldum.
Kwa upande wa Julio Cesar amejiwekea rekodi ya kuwa kipa aliyefungwa mabao 18 katika timu ya taifa ya Brazil katika kushiriki kombe la dunia.
Tatizo la Brazil bado linabaki nafasi ya ulinzi.
Uholanzi wameambulia dola millioni 18 kama washindi wa tatut,Hapo baadaye Ujerumani itacheza na Argentina katika fainali.
0 comments:
Post a Comment