Scolari asema kufungwa kwao si kwa sababu ya Neymar,asema ilikuwa siku mbaya kwake
Baada Jana Usiku Wenyeji Brazil kupewa Kipigo kitakatifu katika Historia ya Kombe la Dunia na Ujerumani ya kubamizwa mabao 7-1 katika Mechi ya Nusu Fainali, Kocha wa Brazil Fillipe Scolari ameeleza kuwa ni ‘Siku mbaya sana katika maisha yake’ na amekubali lawama zote.
Kwenye Mechi hiyo, Ndani ya Nusu Saa, Ujerumani walikuwa mbele kwa mabao 5-0.
Scolari, ambaye alishinda Kombe la Dunia
na Brazil Mwaka 2002, alisema: “Nitakumbukwa kama Kocha aliyefungwa 7-1
lakini nilijua hatari yake nilipokubali kazi hii. Mtu anayechagua Kikosi,
mbinu ni mimi. Lilikuwa chaguo langu.“
Scolari ameeleza kipigo hicho ni ‘janga!’
Alisema: “Ujumbe wangu kwa Watu wa Brazil ni kuwaomba watusamehe kwa uchezaji huu.”
“Naomba radhi kwamba hatukuweza kufika Fainali na tutajaribu kushinda Nafasi ya Tatu. Bado tunacho kitu cha kupigania.”
Hii Ni mara ya kwanza tangu 1938 kwa Brazil kupoteza Nusu Fainali ya Kombe la Dunia pia Kipigo kikubwa kingine kwa Brazil ni Mwaka 1920 walipochapwa 6-0 na Uruguay
Kwenye Mechi hiyo ya kugombea Mshindi wa
Tatu hapo Jumamosi, Brazil watakutana na Argentina au Uholanzi ambao
Jumatano Usiku wanacheza Nusu Fainali ya Pili ya Kombe la Dunia.
Scolari amekataa kuchukulia kukosekana
kwa Staa wake Neymar na Nahodha wake Thiago Silva kuwa ndio sababu na
kueleza: “Tusitafute kisingizio kwa Neymar. Tulijaribu kadri ya uwezo
wetu na tumekutana na Kikosi cha Ujerumani kilicho bora. Tulishindwa
kujizoa baada kuwa nyuma. Hata Wajerumani hawawezi kukuelezea nini
kilitokea lakini ni sababu ya ufundi wao na lazima uheshimu hilo!”
0 comments:
Post a Comment