Thursday, 17 July 2014

Liverpool yachapwa mchezo wa kujipima nguvu.

Liverpool jana huko Brondby, Denmark walichapwa mabao 2-1 katika Mechi yao ya kwanza ya Ziara yao ya kabla Msimu mpya kuanza walipofungwa na Wenyeji wao Club Brondby IF.
Wakiwa chini ya kochaa wao Brendan Rodgers ambaye Msimu uliopita alifanya kazi kubwa kuisaidia kumaliza Nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Manchester City, Liverpool walichezesha Kikosi mchanganyiko na Kipindi cha Pili kilipoanza kubadili Wachezaji kumi.
Bao la kwanza la Brondby lilifungwa na Christian Norgaard kwenye Dakika ya 24.
Hadi Mapumziko Brondby 1 Liverpool 0.
Liverpool walisawazisha katika Dakika ya 48 kwa Bao la Kristoffer Peterson ambaye aliingizwa kutoka Benchi.
Bao la ushindi kwa Brondby lilifungwa na Mchezaji wao kutoka Macedonia, Ferhan Hasani katika Dakika ya 90.
Hadi mwisho, Brondby 2 Liverpool 1.Mechi inayofuata kwa Liverpool ni dhidi ya Preston Northend hapo Julai 19.

0 comments:

Post a Comment