Van Gaal rasmi mazoezini
Kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal na Kikosi chake cha Wachezaji 25 wametua huko Los Angeles Marekani jana tayari kwa Ziara yao ya kabla Msimu mpya kuanza.
Wakiwa
wamefikia Hoteli ya Beverly Hills, Louis van Gaal alikichukua Kikosi
chake kuzunguka Bichi ya Santa Monica ili kunyoosha miguu baada ya
safari ndefu kutoka Jiji la Manchester.
Huko Marekani, Man United watacheza Mechi 4 na ya kwanza ni Julai 23 dhidi ya LA Galaxy ya USA kuwania Chevrolet Cup.
Baada ya hiyo watapambana na AS Roma, Inter Milan na Real Madrid
kuwania International Champions Cup na wakifuzu kuingia Fainali
watacheza Mechi yao ya 5 huko Marekani hapo Agosti 4.
Mechi ya kwanza kwa Van Gaal Uwanja wa Nyumbani Old Trafford ni dhidi
ya Valencia hapo Agosti 12 na Siku 4 baadaye wataanza Msimu mpya wa Ligi
Kuu England kwa kuivaa Swansea City pia Uwanja wa Old Trafford.
Kikosi cha Man United kilianza Mazoezi Julai 4 chini ya Meneja
Msaidizi Ryan Giggs na Makocha wapya walioletwa na Van Gaal, Albert
Stuivenberg, Marcel Bout na Kocha wa Makipa Frans Hoek.
Wachezaji ambao bado hawajajiunga na Kikosi hicho baada ya kupewa
muda zaidi wa Mapumziko baada kuwa huko Brazil kwenye Fainali za Kombe
la Dunia ni Robin van Persie, Marouane Fellaini na Javier Hernandez
‘Chicharito’.
Pia Michael Carrick na Anderson wamekosekana kwa sababu ni majeruhi
huku Patrice Evra akiachwa kwa sababu ya matarajio ya Uhamisho wake
kwenda Juventus.
Akizungumzia Mazoezi ya Timu yake, Van Gaal alisema kumekuwa na ugumu
kutokana na Wachezaji kurudi Klabuni kwa wakati tofauti kutokana na
Kombe la Dunia na hivyo wamepaswa kuwapa Mazoezi kibinafsi zaidi.
Lakini Mchezaji mpya wa Man United, Ander Herrera, amesema: “Hizi
Wiki za kwanza zimekuwa safi. Mazoezi ni mazuri, sawa na Athletic
Bilbao, ambako tunafanya mazoezi sana na Mpira. Makocha wanataka
tumiliki Mpira na kuudhibiti na hili ni safi kwa sisi Wachezaji!”
|
0 comments:
Post a Comment