Sunday, 20 July 2014

Taifa Stars dimbani leo,Uganda mambo yao safi walishinda 2-0

Timu ya taifa ya soka Tanzania Taifa Stars, chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij, inatarajia kucheza  leo (Julai 20) dhidi ya Msumbiji  kuwania kupangwa hatua ya makundi ili kusaka tiketi ya fainali za AFCON zitakazochezwa Morocco hapo mwakani.
Taifa Stars imewasili juzi Dar es salaam ikitokea Mbeya ambapo iliweka kambi kwa ajili ya mchezo huo.
Taifa Stars ilitoa Zimbabwe kwa jumla ya mabao 3-2 katika hatua iliyopita na  Viingilio kwa mechi hiyo  itakayochezwa leo (Jumapili) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni sh. 7,000 na sh. 30,000 kwa viti maalumu 45,000 tu.
Mashindano yalianza kunguruma jana jumamosi  ambapo Botswana, Uganda na Sierra Leone wameshinda michezo yao ya awali. Botswana iliwachapa Guinea-Bissau 2-0 ikiwa nyumbani kwao  Gaborone.
Lemponye Tshireletso alifunga mabao yote mawili kwa upande wa Botswana.
Lakini baada ya mchezo kumalizika kocha wa  Botswana Peter Butler alikiri kuwa wapinzani walikuwa wakali ila wao wametumia nafasi walizopata.
Naye kocha wa Guinea-Bissau  Paulo Torres amesisitiza kuwa watajitahidi katika mchezo wa marudiano.
MATOKEO YA JANA JUMAMOSI
  • Botswana 2-0 Guinea-Bissau
  • Uganda 2-0 Mauritania  Shelisheli
  • LEO JUMAPILI
  • Lesotho v Kenya
  • Tanzania v Msumbiji
  • Congo Brazzaville v Rwanda 
  • Benin v Malawi 
Katika michezo mingine  Uganda iliwabamiza  Mauritania 2-0 jijini Kampala.
Brian Majwega alifunga bao la kwanza dakika ya  49.
Geofrey Massa, anayechezea klabu ya University of Pretoria ya Afrika kusini alifunga bao la pili
Sierra Leone ilishinda mbele ya  Shelisheli 2-0 mjini Freetown.
Khalifa Jabbie alifunga bao la kwanza dakika ya 56. Umaru Bangura aliongeza bao la pili kabla ya filimbi ya mwisho.
Michezo ya marudiano itapigwa kati ya Agosti1-3. Michezo ya AFCON 2015 Morocco itachezwa kuanzia Januari 17 hadi  Februar 8 2015.  

0 comments:

Post a Comment