Monday, 14 July 2014

Manchester United na Adidas zakubaliana mkataba mnono,mkataba ni balaa dunia nzima.

Klabu ya Manchester United Leo hii imetangaza kufikia makubaliano na Kampuni ya Adidas ya Miaka 10 ya Jezi na Vifaa vya Michezo ambapo watalipwa €940 million na hii ndiyo Dili kubwa Duniani kwa Mikataba ya aina hiyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa Goal.com Mkataba wa pande hizo mbili utaanza Msimu wa Mwaka 2015/16 na kila Mwaka Man United italipwa Pauni Milioni 94 ikiipita Real Madrid ambayo ilikuwa ikizoa Pauni Milioni 31 kwa Mwaka pia kutoka kwa Adidas.
Taarifa hiyo imeendelea kudai zaidi kuwa Msimu huu unaokuja, wa 2014/15, Man United itamaliza Mkataba wa kuvaa Jezi za Nike ambazo wamekuwa nazo kwa Miaka 13 hadi sasa.
Mkurugenzi mtendaji wa Adidas Herbert Hainer amesema kuwa wamevutiwa na klabu hiyo,amabpo amedai kuwa ni timu bora na inayopendwa na watu wengi duniani.
DILI KUBWA ZA JEZI:
TIMU
KAMPUNI
KWA MWAKA
MIAKA
JUMLA
Manchester United
Adidas
£94m
10
£940m
Real Madrid
Adidas
£31m
8
£248m
Chelsea
Adidas
£30m
10
£300m
Arsenal
Puma
£30m
5
£170m
Barcelona
Nike
£27m
10
£270m
Liverpool
Warrior
£25m
6
£150m
Manchester City
Nike
£12m
6
£72m

0 comments:

Post a Comment