CBF imetangaza rasmi kuwa Scolari ameacha kazi.
Baada taarifa kutoka Brazil kutapakaa kuhusu kutimuliwa kwa Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari hapo Jana, hatimaye Shirikisho la Soka la Brazil,CBF limetoa tamko kwamba Kocha huyo ameamua kuiacha nafasi yake.Hata hivyo, Mkataba wa Scolari ulikuwa unamalizika mara baada ya Fainali za Kombe la Dunia kuisha.
Kocha huyo mwenye miaka 65 hapo awali aligoma kujiuzulu baada ya kufungwa mabao 7-1 na Ujerumani na mwishoni mwa wiki iliyopita aliwahi kusema anawaachia maamuzi hayo CBF ili kumjadili.
Hata hivyo CBF jana walipokea barua ya Scolari.
Brazil maarufu kama Selecao waliianza vyema mashindano lakini kadri mashindano yalivyokuwa yanafikia mwishoni walishindwa kuhimili vishindo..
Brazil walichapa Croatia katika mchezo wa ufunguzi na kwenda sare dhidi ya Mexico. Walishinda mbele ya Cameroon na kuingia hatua ya mtoano na walifunga Chile kwa taabu kabla ya kuwashindilia Colombia 2-1 katika robo fainali.
Ndoto za wenyeji kutinga fainali zilizimwa na Ujerumani baada ya kudhalilishwa 7-1 kabla ya kubamizwa na Uholanzi mabao 3-0 katika kumtafuta mshindi wa tatu.
Scolari ameiongoza Brazil kushinda michezo 19 katika mipambano 29 baada ya mara ya pili kuifundisha timu hiyo na kubeba kombe la mabara mwaka 2013.
Scolari ndie aliekuwa Kocha wa Brazil Mwaka 2002 walipotwaa Kombe la Dunia kwa mara ya mwisho na hiyo ikiwa mara ya 5 katika Historia yao.
0 comments:
Post a Comment