Sunday, 13 July 2014

Waliowahi kutwaa tuzo ya Golden Ball tokea 1930 hwa hapa

Fainali za kombe la dunia Zitahitimishwa leo kwa mchezo wa fainali kati ya Ujerumani na Argentina na Shirikisho la soka duniani FIFA imetangaza Majina ya Wachezaji 10 watakaogombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil, Tuzo ya Mpira wa Dhahabu.
Listi hiyo ya Wachezaji 10 inao Wachezaji Wanne kutoka Ujerumani, Watatu wa Argentina huku Colombia, Brazil na Uholanzi  zikitoa Mchezaji mmpja moja.
Wachezaji wa Argentina ambao wako kwenye Lisi hiyo ni Angel Di Maria, Javier Mascherano na Lionel Messi.
Ujerumani ni Mats Hummels, Toni Kroos, Phillip Lahm na Thomas Muller.
Waliobaki ni Straika wa Colombia James Rodriguez, Nyota wa Brazil Neymar na Arjen Robben wa Uholanzi.
‘GLOVU YA DHAHABU’
Vile vile FIFA imateja Majina ya Makipa Watatu ambao watawania Tuzo ya Kipa Bora wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.

Manuel Neur
Kipa Bora atapewa Tuzo ya Glovu ya Dhahabu.
Makipa hao ni Kipa wa Costa Rica Keylor Navas, Manuel Neuer wa Germany na Kipa wa Argentina Sergio Romero.
‘MCHEZAJI BORA KIJANA’
Pia, mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay pamoja na Paul Pogba na Raphael Varane wa Ufaransa wameteuliwa kugombea Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana.
Washindi wote wa Tuzo hizo watatangazwa mara baada ya Fainali ya Jumapili kati ya Argentina na Ujerumani  huko Estadio Maracana, Rio de Janeiro.

Waliowahi kutwaa tuzo hizo

1930 Jose Nasazzi (Uruguay)
1934 Giuseppe Meazza (Italy)
1938 Leonidas (Brazil)
1950 Zizinho (Brazil)
1954 Ferenc Puskas (Hungary)
1958 Didi (Brazil)
1962 Garrincha (Brazil)
1966 Bobby Charlton (England)
1970 Pele (Brazil)
1974 Johan Cruyff (Netherlands)
1978 Mario Kempes (Argentina)
1982 Paolo Rossi (Italy)
1986 Diego Maradona (Argentina)
1990 Salvatore Schillaci (Italy)
1994 Romario (Brazil)
1998 Ronaldo (Brazil)
2002 Oliver Kahn (Germany)
2006 Zinedine Zidane (France)
2010 Diego Forlan (Uruguay)

0 comments:

Post a Comment