Sunday, 6 July 2014

Mchezaji aliyeweka rekodi kombe la dunia 2014 astaafu rasmi soka.

Golkipa wa Colombia Faryd Mondragon  aliyeweka rekodi mwaka huu katika mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea kule Brazil kwa kuwa mchezaji aliyecheza akiwa na umri mkubwa amestaafu soka baada ya Colombia kuaga mashindano ya kombe la dunia..

Mondragon mwenye miaka 43 aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza kombe la dunia akiwa na umri mkubwa baada ya kuchukua nafasi ya David Ospina wakicheza na  Japan katika makundi.
Baada ya kutolewa kipa huyo aliandika maneno machache katika ukurasa wake wa instagram "Huu ni uwanja wangu wa mwisho kucheza kama mchezaji wa kimataifa,nina furaha kuwa mmojawapo wa wachezaji waliopo kwenye kundi hili."
Mondragon akimpongeza Ospina kabla ya kuingia,mchezo dhidi ya Japan,kombe la dunia 2014
Sports4lifetz angalau kwa ufupi inakupatia wasifu wa Faryd Camilo Mondragón Alí ambaye alizaliwa  June  21.1971 maeneo ya Cali, Colombia.
Alianza kucheza soka mwaka1990 klabu ya Deportivo Cali ya nchini Colombia
Soma zaidi hapa vilabu alivyochezea
Mwaka Klabu Michezo (mabao)
1990–1991 Deportivo Cali 1 (0)
1992 Real Cartagena 15 (0)
1992 Santa Fe 2 (0)
1993 Cerro Porteño 11 (0)
1993–1994 Argentinos Juniors 21 (0)
1994–1995 Independiente 0 (0)
1995 Santa Fe 30 (0)
1995–1998 Independiente 103 (1)
1999 Real Zaragoza 13 (0)
1999–2000 Independiente 16 (0)
2001 Metz 30 (0)
2001–2007 Galatasaray 185 (0)
2007–2010 1. FC Köln 106 (0)
2011 Philadelphia Union 27 (0)
2012–2014 Deportivo Cali 78 (0)
Jumla
638 (1)
Alianza kuichezea Colombia mwaka 1993–2014 na kucheza michezo 56

0 comments:

Post a Comment