Stars walazimishwa sare na Msumbiji.
Timu ya soka ya Tanzania, Taifa Starssare ya mabao 2-2 na Msumbiji katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco,mchezo huo, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hii leo.Mabao ya Stars inayofundishwa na Mholanzi Mart Nooij yalifungwa na , Khamis Mcha ‘Vialli’ aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa.
Dakika 45 za kwanza zilimalizika bila bao na kipindi cha pili, Msumbiji walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 47 kwa penalti iliyokwamishwa nyavuni na Elias Pelembe baada ya Kevin Yondan kucheza rafu kwenye eneo la hatari. Mcha aliisawazishia Stars bao hilo dakika ya 65 akimalizia kazi nzuri ya Thomas Ulimwengu.
Mcha tena akaifungia Stars bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 71 kwa penalti, baada ya mabeki wa Mambas kumchezea rafu Mbwana Samatta kwenye eneo la hatari.
Msumbiji walizinduka na kufanya shambulizi zuri lililowapatia bao la kusawazisha dakika ya 87 kupitia kwa Isaac Carvalho aliyetokea benchi pia.
Kwa matokeo, hayo Stars sasa itahitaji ushindi wa ugenini ili kusonga mbele, au sare ya kuanzia mabao 3-3, wakati wenyeji wanaweza kunufaika na sare ya 1-1 au 0-0. Ikiwa 2-2 tena, mshindi ataamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

0 comments:
Post a Comment