Mtaalam wa Manchester United astaafu baada ya kuitumikia klabu miaka 23
Mkuu wa Kutibu Viungo wa Manchester United, Rob Swire, amestaafu baada ya kuitumikia Klabu hiyo kwa Miaka 23.
Swire, mwenye Miaka 51 na ambaye amekuwa
akiongoza Kitengo cha Kutibu Viungo [Physiotherapy] cha Man United tangu
Mwaka 1999, alijiunga na Old Trafford Mwaka 1991.
Nafasi ya Swire itachukuliwa na Msaidizi wake Neil Hough ambae yeye mwenyewe ndiye alimteua Miaka 15 iliyopita.
Swire ameamua kwa hiari yake mwenyewe
kustaafu na ameeleza: “Si uamuzi rahisi, ni uamuzi mkubwa. Nimekuwa
nikifikiria hili kwa zaidi ya Mwaka nikitafuta wakati muafaka nistaafu.
Nimefanya kazi hii kwa muda mrefu na bila kuwa na Masaa maalum hivyo
unafanya kazi kila wakati, pamoja na Wikiendi na Jioni na kusafiri sana
na haikuwa rahisi kwa Familia yangu.”
![]() |
| SWIRE akimtibu Beckam mwaka 2000 |
Kadhalika kocha mstaafu wa Man United, Sir
Alex Ferguson, amemsifia sana Swire kwa kusema: “Nakumbuka Rob alipoanza
kazi Klabuni, alikuwa ni Kijana mwenye nia ya kazi yake na anaekazania
kujiboresha zaidi na kujifunza zaidi. Alikuwa mwaminifu mno. Ni Mtu
mzuri na Binadamu safi sana. Sijapata kuwa na tatizo lolote toka kwake.”
Ferguson aliongeza: “Nimefanya kazi na
Rob kwa muda mrefu na nasikia fahari kubwa kwa kazi yake. Ameitumikia
Klabu vyema na namtakia kila la kheri katika maisha yake ya baadae. ”
Kwa upande wake koche Msaidizi wa Man United, Ryan
Giggs, pia amemsifia sana Rob Swire kwa kusema: “Rob amekuwa Mtumishi
mwema mno wa Klabu na yupo hapa muda mrefu. Napenda nimshukuru kwa
msaada wake wote na kuniwezesha mimi kucheza kwa muda mrefu. Amefanya
kazi bila kuchoka kwa manufaa ya Timu na hajapata hata mapumziko.”


0 comments:
Post a Comment