Saturday, 5 July 2014

Equatorial Guinea yatupwa nje na CAF,sababu mchezaji mzaliwa wa Cameroon

Nchi ya  Equatorial Guinea imeondolewa kwenye  mashindano ya kufuzu kuwania tiketi ya ubingwa wa Afrika mwakani huko Morocco,shirikisho la soka la Afrika(CAF) limetangaza ijumaa
Equatorial Guinea Imepatikana na hatia ya kumtumia mchezaji ambaye ni raia wa Cameroon Thierry Fidieu ambaye alicheza nchi ya E.Guinea dhidi ya  Mauritania mwezi  May.Hakuna ushahidi uliotolewa kudhibitisha kuwa Tazemeta alikuwa kabadili Uraia .
Mauritania ilikuwa imeuliza kudhibitishwa kwa uraia wa mchezaji huyo katika mkondo wa kwanza ilipoibuka mshindi wa 1-0.
Equatorial Guinea hata hivyo ilipuuza madai hayo na ikamshirikisha katika mechi ya pili ambayo E .Guinea iliibuka na ushindi mkubwa wa 3-0 .
Kufuatia kauli hiyo Mauritania imerejeshwa mashindanoni na sasa itakabiliana na Uganda katika mkondo wa mwisho wa kufuzu.
Mwaka uliopita Equatorial Guinea ilipoteza mechi mbili kwa sababu sawa na hizo katika mechi ya kufuzu kwa mashindano ya kombe la dunia la Brazil,2014.


0 comments:

Post a Comment