Saturday, 5 July 2014

Neymar nje kombe la dunia

Mchezaji nyota wa Brazil Neymar hatachezea nchi yake mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea kule Brazil kwa mwaka 2014 baada ya kuumia sehemu  inayoshikana na mgongo yaani vertebra na aliumia jana Brazil ikicheza dhidi ya Colombia,ameeleza dakatari wa timu ya Brazil.
Neymar anaangushwa na Zuniga dk ya 88
Nyota huyo wa Brazil ambaye mpaka sasa amefunga mabao manne alikumbana na mchezaji wa Colombia Juan Camilo Zuniga  katika dakika ya  88 ya mchezo huo,atakosa mechi ya Brazil dhidi ya Ujerumani au hatua ya fainali iwapo Brail ikifuzu hapo  July 13.
Dakatari wa timu  Rodrigo Lasmar amesema  Neymar  amevunjika  mfupa wa tatu katika mgongo yaani  vertebra.
Marcelo akilalama kwa mwamuzi baada ya Neymar kuangushwa chini.

"Jeraha hilo halihitaji upasuaji ila kuna matibabu yake maalum"alisema Lasmar
Neymar akisikilizia maumivu
Mapema jana Mabeki mahiri wa klabu ya PSG Inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa Thiago Silva na David Luiz walikuwa shujaa katika mchezo uliomalizika  katika dimba la Castela mjini Forteleza.
Nahodha  Thiago Silva  alifunga bao la kwanza  akipokea mpira kutoka kwa Neymara ambaye aliumia na alishindwa kufurukuta mbele ya Mabeki wa Colombia.
Dakika ya  69 beki David Luiz ambaye kwa sasa amehamia PSG akafunga bao la pili na la ushindi baada ya mpira wa adhabu  mita 30 kutoka langoni.
Thiago Silva atakosa mchezo wa nusu fainali baada ya kupewa kadi ya njano,Brazil itapambana na Ujerumani ambayo imeshinda 1-0 dhidi ya Ufaransa.Baada ya mchezo kumalizika Silva alisema kuwa pengo lake litazibwa katika mchezo unaofuata "Nina furaha kwa sababu nilijitolea kwa moyo wangu kuitumikia timu,sitakuwepo mchezo unaofuata ila Dante na Henrique watacheza vizuri." alisema Silva akihojiwa baada ya mchezo kumalizika.

0 comments:

Post a Comment