Saturday, 5 July 2014

Ratiba ya leo(Julai 5) mpaka fainali

Baada ya Ijumaa (Julai 4) kushuhudiwa Brazil na Ujerumani wakitinga hatua ya nusu fainali,leo kama kawaida ratiba ya michezo hii yenye raha ya aina yake itaendelea kwa timu nyingine kutafuta hatua ya nusu fainali.
Hapo kabla Timu zilizoingia robo fainali ni Wenyaji Brazil, ambao ni Mabingwa wa Dunia mara 5, wapo Mabingwa wengine wa zamani Ufaransa,Ujerumani na Argentina lakini pia zipo timu ambazo hazijawahi kutwaa Kombe hili ambazo ni Colombia, Ubelgiji,Uholanzi na Costa Rica.
Brazil iliingia robo fainali baada ya kuitoa Chile kwa mikwaju ya pelnati vilevile Ujerumani iliitoa Algeria katika muda wa nyongeza wakati Ubelgiji nao iliwachukua mpaka muda wa nyongeza kuwatoa Marekani.
Aidha Costa Rica mikwaju ya pelnati iliwapeleka hatua hii baada ya kuwafunga Ugiriki.
Uholanzi na Ufaransa waliingia baada ya kushinda katika dakika 90 za mchezo,Uholanzi ikiwatoa Mexico wakati Ufaransa iliwachomoa mabingwa wa Afrika Nigeria.
JUMAMOSI, JULAI 5, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Argentina v Ubelgiji [59] ROBO FAINALI Nacional, Brasilia
2300 Uholanzi  v Costa Rica [60] ROBO FAINALI Arena Fonte Nova, Savador
NUSU FAINALI
JUMANNE, JULAI 8, 2014

SAA MECHI KUNDI UWANJA
2300  Ujerumani v Brazil [61] NUSU FAINALI Estadio Mineirão, Belo Horizonte
JUMATANO, JULAI 9, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
2300 Mshindi kati ya Argentina v Ubelgiji v Mshindi kati ya Uholanzi v Costa Rica [62] NUSU FAINALI Arena Corinthians, Sao Paulo
MSHINDI WA TATU
JUMAMOSI, JULAI 12, 2014

SAA MECHI KUNDI UWANJA
2300 Aliyefungwa 61 v Aliyefungwa 62 MSHINDI WA 3 Nacional, Brasilia
FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014

SAA MECHI KUNDI UWANJA
2200 Mshindi Mechi 61 v Mshindi Mechi 62 FAINALI Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

0 comments:

Post a Comment