Nigeria yapigwa stop na FIFA.
Shirikisho la soka Dunianai FIFA imeifungia Shirikisho la Soka la Nigeria, NFF,baada ya shughuli zake kuingiliwa .
FIFA imetoa taarifa kwamba
Kamati ya Dharura imeamua kuisimamisha Nigeria mara moja baada Mahakama
Kuu ya Jos, Plateau State, kusimamisha shughuli za NFF na kumtaka Waziri
wa Michezo wa Nigeria kumteua Mtu kuendesha shughuli za NFF.
FIFA imesema maamuzi hayo ni kinyume na
Kanuni ya 13, Aya ya 1 na Kanuni ya 17, Aya ya 1 ya Sheria za FIFA
ambazo zinataka Vyama vya Wanachama wake kuendeshwa huru na kutoingiliwa
na upande mwingine wowote.
Hapo Julai 4, Katibu Mkuu wa FIFA,
Jerome Valcke, aliiandikia Nigeria na kuipa hadi Julai 8 kuirudisha
Madarakani NFF na kutoingiliwa tena kwa namna yeyote.
Barua ya Valcke iliikumbusha Nigeria
wajibu wake wa kuiruhusu NFF kuendesha shughuli zake bila kuingiliwa na
Mtu yeyote kwa mujibu wa Kanuni ya 13 ya Sheria za FIFA.
Pia Barua hiyo iliionya Nigeria kuwa
endapo NFF haitarejeshwa madarakani ifikapo Julai 8 basi Vyombo husika
vya FIFA vitachukua hatua zaidi ikiwa pamoja na kuisimamisha Nchi hiyo
kwenye shughuli zote za Kimataifa za Soka ikimaanisha kufungiwa kwa Timu
yao ya Taifa na Klabu zao zote kucheza michuano ya Kimataifa.
Uamuzi huu utaifaya Nigeria isiweze kushiriki Mashindano yeyote ya Kimataifa.

0 comments:
Post a Comment