Nilikosa watu wa kwanza wa kupiga pelnati-Van Gaal.
Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal amesema kuwa alipata shida sana kumpata Mchezaji wa kupiga Penalti ya Kwanza ilipofikia hatua ya Mikwaju ya Penati Tano Tano baada Timu yake na Argentina kutoka 0-0 katika Dakika 120 za Nusu Fainali ya Kombe la Dunia hapo Jana.
Kwenye Penalti hizo, Argentina waliibuka
kidedea kwa kushinda Penati 4-2 baada Uholanzi kukosa Penati mbili
zilizopigwa na Ron Vlaar na Wesley Sneijder na Kipa Sergio Romero
kuokoa.
Beki Ron Vlaara ndiye aliepiga Penalti ya Kwanza.
Lakini Louis van Gaal, ambaye Timu yake
iliitoa kwenye Robo Fainali Costa Rica kwa Penalti mbili kati yake
ziliokolewa na Kipa wa Akiba Tim Krul aliyeingizwa Dakika za Mwishoni
kwa ajili tu ya Penati, Jana alishindwa kutumia mbinu hiyo hiyo baada ya
kuwa tayari washabadilisha Wachezaji Watatu.
Akiongea na Wanahabari mara baada ya
Mechi, Van Gaal alisema: “Ile na Costa Rica ingetupa imani kwani
tulipiga vizuri sana. Lakini tatizo lilikuwa nani apige ya kwanza na
niliwaomba Wachezaji Wawili na mwisho nikaangukia kwa Vlaar. Yeye ndiye
alikuwa Mchezaji bora hivyo angekuwa anajiamini mno. Lakini hii
inaonyesha jinsi ilivyokuwa ngumu kupiga Penati kwenye Penati Tano
Tano.”
Aliongeza: “Ni mbaya mno, kupoteza Mechi kwa Penati. Ukiondoa yote, tulikuwa sawa na wao, kama sio Timu bora. Inahuzunisha sana!”
0 comments:
Post a Comment