Mabeki wa PSG waipeleka Brazil nusu fainali,Rodriguez apiga la 6
Timu ya taifa ya Brazil imefuzu hatua ya nusu fainali za kombe la dunia mashindano yanayofanyika kule kwao baada ya kuibugiza timu ngumu ya Colombia mabao 2-1.Mabeki mahiri wa klabu ya PSG Inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa Thiago Silva na David Luiz walikuwa shujaa katika mchezo uliomalizika muda mfupi uliopita katika dimba la Castela mjini Forteleza.
Nahodha Thiago Silva alifunga bao la kwanza akipokea mpira kutoka kwa Neymara ambaye leo alishindwa kufurukuta mbele ya Mabeki wa Colombia.
Dakika ya 69 beki David Luiz ambaye kwa sasa amehamia PSG akafunga bao la pili na la ushindi baada ya mpira wa adhabu mita 30 kutoka langoni,
| Mfungaji wa bao la pili,David Luis |
Thiago Silva atakosa mchezo wa nusu fainali baada ya kupewa kadi ya njano,Brazil itapambana na Ujerumani ambayo imeshinda 1-0 dhidi ya Ufaransa.
![]() |
| ALIFUNGA LA KWANZA,THIAGO SILVA |
Lakini Neymar aliumia na kukimbizwa hospitalini baada ya kukumbana na Juan Camillo Zuniga akilalamika maumivu ya mgongo.


0 comments:
Post a Comment