Sasa ni EURO 2016,makundi haya hapa.
Makundi ya michuano ya Ulaya kwa upande wa Nchi yaani EURO yamepangwa ambapo mabingwa wa dunia Ujerumani watarudi dimbani tena kwenye Mashindano rasmi hapo Septemba 7 kuanza kampeni ya kutinga Fainali zitakazochezwa huko Ufaransa Mwaka 2016.Ujerumani , ambao wako Kundi D la EURO 2016, wataanza kucheza Nyumbani na Scotland.
Kabla ya Mechi hiyo, Ujerumani watacheza Mechi ya Kirafiki huko Dusseldorf hapo Septemba 3 na Argentina, Timu ambayo ndiyo waliibwaga kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Maracana, Rio de Janeiro, Nchini Brazil kwa Bao 1-0
Mechi hii ya Kirafiki ilipangwa kabla hata ya kujulikana kama Nchi hizo zitakutana Fainali ya Kombe la Dunia.
Baada ya kuanza na Scotland, Mechi nyingine za Kundi D kwa Ujerumani ni dhidi ya Poland, Jamhuri ya Ireland, Gibraltar na Georgia.
Uholanzi, ambao walimaliza Nafasi ya Tatu kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil, wako Kundi A na wataanza na Czech Republic hapo Septemba 9 lakini safari hii watakuwa chini ya Kocha mpya, Guus Hiddink, anayerithi mikoba ya Louis van Gaal ambaye amehamia kuwa Meneja mpya wa Manchester United.
Uingereza wao wako Kundi E na wataanza Ugenini na Switzerland hapo Septemba 8.
Mechi za Ufunguzi za EURO 2016 zitachezwa kwa Siku 3 mfululizo kuanzia Septemba 7 hadi Septemba 8.
Wenyeji Ufaransa wao hawamo kwenye Makundi wanatarajiwa kucheza Mechi ya Kirafiki hapo Septemba 7 dhidi ya Serbia.
Timu mbili za juu toka kila Kundi pamoja na Timu moja Bora iliyoshika Nafasi ya 3 kwenye Makundi zitatinga Fainali na Timu 8 zilizobaki ambazo zitamaliza Nafasi ya Tatu zitapangiwa Mechi maalum za Mchujo ili kupata Timu 4 za mwisho kuingia Fainali.
Mechi za Makundi zitaanza Septemba 2014 hadi Oktoba 2015 na Ratiba kamili itatolewa na UEFA baada ya Droo.
Fainali za UEFA EURO 2016 zitachezwa Nchini Ufaransa kuanzia Juni 10, 2016 hadi Julai 10, 2016 na kwa mara ya kwanza Fainali hizo zitakuwa na Nchi 24 badala ya zile 16 za kawaida.
KUNDI A: Uholanzi, Czech Republic, Uturuki, Latvia, Iceland, Kazakhstan.
KUNDI B: Bosnia-Hercegovina, Ubelgiji, Israel, Wales, Cyprus, Andorra.
KUNDI C: Hispania, Ukraine, Slovakia, Belarus, FYR Macedonia, Luxembourg.
KUNDI D: Ujerumani, Jamhuri ya Ireland, Poland, Scotland, Georgia, Gibraltar.
KUNDI E: Uingereza Switzerland, Slovenia, Estonia, Lithuania, San Marino.
KUNDI F: Ugiriki, Hungary, Romania, Finland, Ireland ya kaskazini , Faroe Islands.
KUNDI G: Urusi, Sweden, Austria, Montenegro, Moldova, Liechtenstein.
KUNDI H: Italia, Croatia, Norway, Bulgaria, Azerbaijan, Malta.
KUNDI I: Ureno, Denmark, Serbia, Armenia, Albania.
0 comments:
Post a Comment