Watu mbalimbali kwenye picha wakiwa katika maombolezo ya kifo cha Di Stefano.
Waombelezaji leo wameendelea kutoa heshima zao kwa aliyekuwa gwiji wa klabu ya Real Madrid Alfredo Di Stefano Wakati jeneza lake liliwekwa katika uwanja wa
Bernabeu.
Di Stefano alifariki jana akiwa hospitalini akiwa na umri wa miaka 88,baada ya kupata mshtuko wa moyo.

Alfredo Di Stefano:
Di Stefano alianza kucheza soka akiwa na klabu ya River Plate baadaye akajiunga na Madrid akitokea klabu iliyopo nchini Colombia, Millonarios Mwaka 1953, kabla ya hapo alikaribia kujiunga na Barcelona.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Argentine aliitumikia Madrid kushinda mataji 8 ya Liga na mataji 5 ya ligi ya mabingwa kati ya 1953 na 1964.
Amefunga mabao 308 katika michezo 396 kwa upande wa Real na nabaki kuwa mfungaji bora wa pili wa Madrid nyuma ya Raul (323). Mchezaji bor wa dunia Cristiano Ronaldo ameandika katika twita yake kuwa gwiji hafi daima,tunakushukuru.

Rais Florentino Perez wa Real Madrid akisimama karibu na jeneza ambalo lina mwili wa marehemu Alfredo Di Stefano

Watu wakitoa heshima zao

FFamilia na marafiki wakitoa heshima zao hii leo

Mshabiki huyu akiandika ujumbe kama kumbukumbu kwa ajili ya gwiji wao .

Kipa wa Real Madrid Iker Casillas alikuwepo kwenye maombolezo ya marehemu Di Stefano
0 comments:
Post a Comment