Sitamwita kikosini Boateng asema Appiah
Kocha wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah hatamwita mchezaji Kevin-Prince Boateng katika kiosi cha Ghana kwa hapo baadaye baada ya kutolewa kombe la dunia.Ghana imetua nchini kwao jana Baada ya kutolewa na kocha Appiah amesema sasa atachagua wachezaji wenye nidhamu,wanaojituma na walio tayari kufa kwa ajili ya nchi yao.
"Kwa sasa, Kevin-Prince Boateng si sehemu tena ya mipango yangu," alisema Appiah.
Mapema wiki iliyopita Shirikisho la soka nchini Ghana, lilithibitisha kufuzwa kwa wawili hao ambao walikuwa katika kikosi cha “ The Black Stars” na kushiriki katika michuano miwili iliyopita.
Boateng alitumia maneno makali na ya kumkejeli kocha Kwesi Appiah huku Muntari akimvamia na kumjeruhi afisa wa Kamati ya shirikisho la soka GFA.
Walirudishwa nyumbani muda mfupi tu kabla ya Ghana kuvaana na Ureno katika mchuano muhimu wa kumalizia hatu aya makundi.
"Ninapendelea sana kuwa na hali ya nidhamu japo ni kazi ngumu ila sipendelei tabia hii," aliongeza Appiah.
Kocha huyo hakupenda kulizungumzia suala la Muntari.

0 comments:
Post a Comment