Tuesday, 8 July 2014

Maximo ameamua mwaka huu,kuongea na wanahabari kila siku Ijumaa.

Kocha mkuu wa timu ya Young Africans SC Mbrazil Marcio Maximo amesema atakua akiongea na waandishi wa habari kila siku ya Ijumaa asubuhi mara tu baada ya mazoezi katika shule ya sekondari Loyola ili kuwapa fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na maandalizi ya kikosi chake msimu ujao,  taarifa kwa mujibu wa mtandao wa Yanga.

Maximo amesema, ameamua kufanya hivyo ili kupunguza kuwepo taarifa tofauti kuhusiana na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wake katika maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015.

Unajua utendaji wa kazi umebadilika, nafasi yangu kwenye klabu na nilipokua timu ya Taifa ni tofauti, hivyo nimekubaliana na uongozi na umeniruhusu kuwa naongea na vyombo vya habari kwa pamoja kila siku ya Ijumaa mara tu baada ya mazoezi ya asubuhi "alisema Maximo"

Yanga imewaomba Waandishi wa habari, Vyombo vya Habari  kuhudhuria kila siku ya ijumaa shule ya sekondari Loyola ili wapate nafasi ya kuongea na kocha Maximo na kumuuliza maswali, kwani kwa sasa yeye ndiye atakayekua akiongelea timu, wachezaji pamoja na benchi lake la ufundi. 
 
Maximo ameanza kazi ya kukinoa kikosi cha Young Africans tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwatuvia wapenzi, washabik na wanachama ambao wamekua wakijitokeza kwa wingi kushuhudia ufundishaji wa kocha huyo mwenye mvuto mkubwa kwenye soka la Tanzania.

0 comments:

Post a Comment