Saturday, 19 July 2014

Uganda,Botswana na Siera Leone waanza vizuri kufuzu AFCON,Tanzania kesho.

Mashindano  ya kufuzu mashindano ya Afrika,AFCON  2015 Nchini  Morocco yameanza kunguruma hii leo ambapo Botswana, Uganda na Sierra Leone wameshinda michezo yao ya awali.
Botswana iliwachapa Guinea-Bissau 2-0 ikiwa nyumbani kwao  Gaborone.
Lemponye Tshireletso alifunga mabao yote mawili kwa upande wa Botswana.

Lakini baada ya mchezo kumalizika kocha wa  Botswana Peter Butler alikiri kuwa wapinzani walikuwa wakali ila wao wametumia nafasi walizopata.
Naye kocha wa Guinea-Bissau  Paulo Torres amesisitiza kuwa watajitahidi katika mchezo wa marudiano.
MATOKEO YA LEO JUMAMOSI
  • Botswana 2-0 Guinea-Bissau
  • Uganda 2-0 Mauritania  Shelisheli
  • KESHO JUMAPILI
  • Lesotho v Kenya
  • Tanzania v Msumbiji
  • Congo Brazzaville v Rwanda 
  • Benin v Malawi 
katika michezo mingine  Uganda iliwabamiza  Mauritania 2-0 jijini Kampala.

Brian Majwega alifunga bao la kwanza dakika ya  49.
Geofrey Massa, anayechezea klabu ya University of Pretoria ya Afrika kusini alifunga bao la pili
Sierra Leone ilishinda mbele ya  Shelisheli 2-0 mjini Freetown.
Khalifa Jabbie alifunga bao la kwanza dakika ya 56. Umaru Bangura aliongeza bao la pili kabla ya filimbi ya mwisho.
Michezo ya marudiano itapigwa kati ya Agosti1-3. Michezo ya AFCON 2015 Morocco itachezwa kuanzia Januari 17 hadi  Februar 8 2015.

0 comments:

Post a Comment