Sunday, 20 July 2014

Gourcuff kocha mpya Algeria,mkataba kumalizika kombe la dunia 2018 Urusi.

Mfaransa  Christian Gourcuff  ametajwa kuwa ndiye kocha  wa timu ya taifa ya Algeria akichukua mikoba ya Vahid Halilhodzic ambaye aliifikisha Algeria katika hatua ya 16 bora kombe la dunia 2014 nchini Brazil..
Gourcuff alihusishwa sana kuchukua timu hiyo baada ya kombe la dunia ambapo  viongozi wa shirikisho la soka la Algeria A.F.F wamethibitisha rasmi baada ya kikao cha jumamosi hii mjini  Algiers.
Shirikisho hilo limesema kuwa kocha huyo mwenye miaka 59 ataanza kazi rasmi Agosti 1 mwaka huu.
Mkataba wake utamalizika baada ya kombe la dunia 2018 nchini Urusi.
Kwa mantiki hiyo kocha huyu atakuwepo mpaka mashindano ya Afrika mwaka  2015 na  2017.
Kwa mara ya mwisho Gourcuff alikuwa kocha wa klabu ya Lorient,ila aliachia ngazi mwezi mei mwaka huu,pia alishwahi kuwa kocha wa klabu ya  Le Mans na Stade Rennes.
Ataanza kuiongoza Algeria mchezo dhidi ya Ethiopia mwezi septemba ili kufuzu AFCON 2015
Halilhodzic, ambaye aliacha kazi kwa sasa ni kocha wa  Trabzonspor ya nchini Uturuki.

0 comments:

Post a Comment