Wednesday, 27 August 2014

Baada ya Gerard kustafu soka la kimataifa Nahodha wa Uingereza kutajwa kesho.

Baada ya Steven Gerard na Frank Lampard kutangaza kustaafu soka la kimataifa Kocha wa Uingereza Roy Hodgson anatarajiwa kumtangaza Nahodha mpya Alhamisi Mchana.
Gerrard alistaafu kuichezea Uingereza Mwezi Julai mara tu baada ya Nchi hiyo kutupwa nje ya hatua ya Makundi ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.

Vilevile jana nahodha msaidizi Lampard alitangaza kustaafu soka la kimataifa .
Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney, mwenye Miaka 28, ndiye anatajwa sana kukamata wadhifa huo ambao ulikuwa ukishikiliwa na Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, mwenye Miaka 34.

Rooney aliteuliwa mwanzoni mwa mwezi huu na Van Gaal kuwa Nahodha wa Klabu ya Manchester United kukamata wadhifa uliokuwa ukishikiliwa na Nemanja Vidic aliyehamia Inter Milan.

Uingereza  wanatarajiwa kucheza Mechi ya Kirafiki Septemba 3 katika uwanja wa Wembeley dhidi ya Norway na kisha Septemba 8 watacheza Ugenini na Switzerland katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi E la EURO 2016 kusaka nafasi za kucheza Fainali huko Ufaransa.

0 comments:

Post a Comment