Thursday, 28 August 2014

Baada ya Ghana,Tanzania na Kenya Kujitosa AFCON 2017,Misri watuma maombi.

Shirikisho la soka nchini Misri (EFA) limetangaza  nia ya kuandaa michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za AFCON 2017, Baada ya  Shirikisho la Soka Africa kuwanyang’anya Libya Uenyeji

CAF ilifuta Uenyaji wa Libya kutokana na Vita inayoendelea Nchini humo ambayo imesababisha kutojengwa kwa Viwanja vilivyoahidiwa kwa ajili ya Fainali hizo zinazoshirikisha Nchi 16

Taarifa ya mtandao wa EFA kupitia Sports4lifetz imeeleza kuwaMisri imesema kuwa ina kila sababu ya kuandaa michuano hiyo kwa kuwa iliwahi kuanda mwaka 2006 .
Rais wa EFA Hassan Farid amesema kuwa miundombinu inawaruhusu kuomba mashindano hayo.

Misri  mojawapo ya nchi za Afrika Kakazini ina viwanja vizuri vya soka  mfano uwanja wa  Alexandria, uwanja wa Haras El Hedoud  na uwanja wa  Borg Al Arab. Pia kuna viwanja viwili vinavyomilikiwa na jeshi nchini humo.
Pale mjini Cairo kuna viwanja kama uwanja wa kimataifa wa Cairo, uwanja wa Arab Contractors, uwanja  wa Air Defence.

Ikimbukwe jana Ghana pia imeomba kuandaa AFCON 2017  ikiungana na Tanzania,Ethiopia na Kenya.

0 comments:

Post a Comment