Mshambuliaji Samuel Eto'o astaafu soka la kimataifa.
Mchezaji wa kimataifa wa Cameroon maarufu kama Indomitable Lions ,Samuel Eto'o ametangaza kustaafu soka la kimataifa.
Mfungaji huyo wa kihstoria nchini Cameroon ambaye amefunga mabao 56 ametangaza kupitia mtandao wake wa instergram.
Ikiumbukwe kuwa mapema wiki kocha wa timu ya taifa ya Cameroon Volker Finke alitangaza kikosi chake kwa ajili ya kufuzu AFCON 2015 michezo dhidi ya DR Congo hapo September 6 na Ivory Coast September 10 bila ya nahodha wake Samuel Eto’o.
Wachezaji wengine waliotemwa ni Aurelien Chedjou, Benoit Assou-Ekotto, Jean II Makoun, Achille Webo na Charles Itandje wakati mchezaji wa Barcelona Alexandre Song anatumikia adhabu ya michezo mitatu baada ya kufanya makosa kombe la dunia 2014 kule nchini Brazil.
Nyota huyo wa zamani wa Barcelona, Inter na Real Madrid alianza kuitumikia nchi mwaka 1997 na walifungwa mabao 5-0 na Costa Rica.
Mchezo wa mwisho ndani ya kikosi cha Indomitable Lions ni dhidi ya Mexico katika fainali za kombe la dunia,

0 comments:
Post a Comment