EL Merreikh mabingwa kombe la Kagame.
Klabu ya El Merreikh ya Sudan imetwaa Ubingwa wa Klabu za Afrika Mashariki na Kati baada ya kuifunga Bao 1-0 Wenyeji APR,mchezo uliopigwa jana.Bao pelee lilifungwa na Allan Wanga huko Kigali, Rwanda.
Bao hilo la ushindi la Wanga lilifungwa katika Dakika ya 24 na kuwapa El Merreikh Kombe na kitita cha Dola 30,000.
APR baada ya kushika nafasi ya pili imeambulia Dola 20,000.
Polisi ya Rwanda ilitwaa Nafasi ya 3 baada ya kutoka Sare 1-1 na KCC FC ya Uganda na kuiangusha kwa Penati 4-2 na kutwaa kitita cha Dola 10,000.
Mashindano haya, ambayo hufadhiliwa na Rais Kagame, yalianza huko Kigali, Rwanda hapo Agosti 8 na kuhitimishwa jana Agosti 24
0 comments:
Post a Comment