Monday, 25 August 2014

Klabu bingwa Afrika TP Mazembe kucheza na Setif nusu fainali,pata ratiba

Baada ya kutoka sare dhidi ya AS Vita mjini  Kinshasa, klabu ya TP Mazembe  imemaliza ikiwa katika nafasi ya kwanza katoka kundi la  A na kuingia hatua ya nusu fainali ligi ya mabingwa barani  Afrika.

AS Vita ilicheza bila mchezaji wake  Dady Birori.Mchezaji huyo alifungiwa na CAF baada ya kutumia majina mawili tofauti akiwa na klabu yake vilevile timu ya taifa ya Rwanda..
Kosa hilo la Birori limewafanya   Rwanda kunyang'anywa nafasi ya kufuzu AFCON 2015.

Yunus Junior Ssentamu, ambaye alifunga mabao dhidi ya  Zamalek majuma mawili yaliyopita, alishindwa kufurukuta jana japo aliwafanya mabeki wa  TP Mazembe  kukosa amani
Timu hizo zote za  DRC zimemaliza zikiwa katika nafasi za juu lakini TP Mazembe ina mabao mengi ya kufunga

Kutoka Kundi B, Club Sportif Sfaxien ya Tunisia na Entente Sportive de Sétif ya Algeria pia zipo Nusu Fainali.
Ratiba ya nusu fainali
ES Setif (Algeria) v TP Mazembe (DRC)
AS Vita (DRC) v CS Sfaxien (Tunisia)
Mchezo wa kwanza: Septemba 9-21, mchezo wa marudiano Septemba 26-28.

Kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho, kutoka Kundi A, Coton Sports ya Cameroon  na AC Leopards de Dolisie ya Congo zimeingia Nusu Fainali na Kundi B ni Al Ahly ya Misri na Sewe Sports ya Ivory Coast.

Ratiba ya nusu fainali
20 September 2014
Coton Sport (Cameroon)    v    Al Ahly (Egypt)        
Sewe Sport (Ivory Coast)    v    AC Leopards (Congo)

0 comments:

Post a Comment