Hayatou ataka uchunguzi ufanyike baada ya mchezaji kuuawa nchini Algeria.
Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Issa Hayatou Amesema kuwa uchunguzi ufanyike mara baada ya mchezaji Albert Ebosse kuuawa.Mchezaji huyo raia wa Cameroon amefariki dunia akiwa hospitali baada ya kupigwa na kitu kilichorushwa kutoka jukwaani wakati wa mechi ya Ligi ya Algeria, timu yake JS Kabylie,juzi.
Hayatou amesema kuwa hatua kali zichukulie dhidi ya uhalifu huo uliofanyika na kuongeza kuwa uhalifu huo haukubaliki barani Afrika.
Naye rais wa shirikisho la soka la Algeria Mahfoud Kerbadj aliyekwepo uwanjani amesema mauaji hayo ni jambo la hatari nchini Algeria.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alipigwa na kitu hicho kigumu mwishoni mwa mchezo kati ya JS Kabylie na USM Alger mjini Tizi Ouzou.
Taarifa katika tovuti ya Kabylie imesema: "Wizara ya Mambo ya Ndani na Serikali ya Nyumbani, kupitia Waziri Tayeb Belaiz, imeagiza uchunguzi wa wazi uanze mara moja juu ya tukio hilo lililosababisha kifo cha Albert Ebosse.
Ebosse aliifungia bao Kabylie katika mechi hiyo iliyoisha kwa kipigo cha nyumbani cha 2-1 kutoka kwa USM Alger.
0 comments:
Post a Comment