Eto'o atua rasmi Everton miaka miwili.
Aliyekuwa nahodha wa zamani wa Cameroon Samuel Eto'o amesaini mkataba wa Miaka Miwili wa Kuitumikia klabu ya Everton.Eto’o, mwenye Miaka 33, amejiunga kama Mchezaji huru baada ya Mkataba wake na Chelsea wa Mwaka mmoja kumalizika.
Kabla ya mtukutu Mario Baloteli kutua Liverpool klabu hiyo ilikuwa inamhitaji Eto'o.
Eto’o, ambaye amewahi kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika mara 4, alijiunga na Chelsea kutokea Klabu ya Urusi Anzhi Makhachkala Msimu uliopita na kuifungia mabao 12 katika Mechi 34 alizocheza.
Mapema wiki hii kocha wa timu ya taifa ya Cameroon Volker Finke alitangaza kikosi chake kwa ajili ya kufuzu AFCON 2015 michezo dhidi ya DR Congo hapo September 6 na Ivory Coast September 10 bila ya nahodha wake Samuel Eto’o.
Wachezaji wengine waliotemwa ni Aurelien Chedjou, Benoit Assou-Ekotto, Jean II Makoun, Achille Webo na Charles Itandje wakati mchezaji wa Barcelona Alexandre Song anatumikia adhabu ya michezo mitatu baada ya kufanya makosa kombe la dunia 2014 kule nchini Brazil.
Vilevile jana kocha huyo alkimtangaza Stephane Mbia kuwa nahodha kuchukua mikoba ya Eto'o ambaye ameichezea timu ya taifa Miaka 17.
Eto’o alianzia Soka lake huko Real Madrid lakini alipelekwa Malorca na baadaye akaitumikia FC Barcelona.
Akiwa na Barcelona, Eto’o alitwaa Ligi ya mabingwa barani UlayaI mara mbili, Miaka ya 2006 na 2009 huku akipiga Bao katika Fainali hizo zote, na La Liga mara 3 na kisha kuhamia Inter Milan Mwaka 2009 na kutwaa UEFA katika Msimu wake wa kwanza tu.
0 comments:
Post a Comment