Wednesday, 27 August 2014

Ligi ya mabingwa Ulaya,Arsenal bila ya Giroud kucheza na Besiktas.

Ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya mtoano itaendelea kunguruma leo katika viwanja vitano.

Klabu ya Arsenal itakuwa nyumbani kucheza na Besiktas na mchezo wa kwanza timu zilitoka suluhu.

Arsenal wanahitaji ushindi tu ili kufuzu kwani Sare yeyote ya Magoli itamaanisha Besiktas ndio wataingia hatua ya Makundi ya UEFA ambayo Droo yake itafanyika huko Monaco Siku ya Alhamisi.

Mchezaaji Aaron Ramsey ambaye alipewa Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya Kwanza huko Instanbul hatacheza hii leo
Vilevile  Nahodha wao Mikel Arteta mwenye tatizo la Enka na  Olivier Giroud ambaye pia ameumia Enka hawatacheza.

Kocha Wenger aikabidi awatumie Wachezaji Yaya Sanogo au Lukas Podolski au Alexis Sanchez ili kuziba pengo la Giroud.

Kuelekea mchezo huo Jack Wilshere ana uhakika kuwa sare waliyopata dhidi ya Everton itawasaidia katika mchezo.

Hiyo inakuwa mara ya kwanza kwa Arsenal katika mechi 13 walizocheza za mtoano kushindwa kushinda. Lakini Arsenal sasa wanajisikia vyema baada ya kufanikiwa kutoka nyuma kwa kufungwa mabao 2-0 na kufanikiwa kutoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Everton Jumamosi iliyopita.

Akihojiwa Wilshere amesema alama waliyopata dhidi ya everton ilikuwa ni muhimu kwani inawapa nguvu kwa ajili ya mchezo huo.

Wakati Besiktas wana Kikosi kamili na Straika wao Demba Ba yu tayari kurejea tena Jijini London kuitesa Arsenal kama alivyokuwa akifanya akiwa na Klabu yake ya zamani Chelsea, Klabu hiyo ya Uturuki itakuwa bila ya Meneja wao kutoka Croatia kwenye Benchi, Slaven Bilić, ambaYe alipewa Kadi Nyekundu katika Mechi ya Kwanza na hivyo kulazimika kukaa Jukwaani kwa Mechi hii.

MECHI ZA LEO
Jumatano Agosti 27
Arsenal v Besiktas
Athletic Bilbao v Napoli
Bayer 04 Leverkusen v FC Copenhagen
Ludogorets Razgrad v Steaua Bucharest
Malmö FF v FC Red Bull Salzburg





0 comments:

Post a Comment