Mshabiki wa Manchester City aliyeng'atwa na wa Liverpool anaendelea vizuri.
Yule mshabiki wa Manchester City aliyeng'atwa na mshabiki wa Liverpool wakati mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza Ukiendelea juzi mchezo kati ya Manchester City na Liverpool anaendelea vizuri.Ibrahim Ntonga Haruna aliyeng'atwa shavuni amezungumza na mtandao huu na kusema kuwa anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu na kuongeza kuwa amemsamehe yule mshabiki wa Liverpool.
Tukio hilo limetokea katika kata ya Goweko wilayani Uyui mkoani hapa ambapo Zola Gadaffi mshabiki wa klabu ya Liverpool nchini Tanzania alimng'ata mshabiki wa Manchester City bwana Ibrahim Ntonga Haruna eneo la shavuni.
Tukio hilo ambalo liliwashangaza mashabiki wengi katika ukumbi moja kule Uyui lilianza pale Ibrahim Haruna aliposhangilia bao la tatu lililofungwa na Sergio Aguero na kumchukiza Zola Gadafi ambaye aliruka moja kwa moja mpaka shavuni.
Wakati mashabiki wa Italia wakiwa na kumbukumbu ya aliyekuwa mchezaji wa Liverpool Luis Suarez kumng'ata meno Beki Chiellini wa Italia,sasa ni zamu ya mshabiki huyo wa Liverpol kugeuka kuwa Suarez.
Wadau waliokuwepo ukumbini pale waliamua ugomvi huo na jana asubuhi Ibrahim Haruna aliweza kufika hospitalini ili kupata matibabu.
Bwana Haruna amesema kuwa amemsamehe rafiki yake huyo Zola kwa kuwa yale ni mambo ya soka.

0 comments:
Post a Comment