Ghana kama Tanzania itapeleka maombi kuandaa AFCON 2017.
Shirikisho la soka nchini Ghana limetangaza nia ya kuandaa michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za AFCON 2017, Baada ya Shirikisho la Soka Africa kuwanyang’anya Libya Uenyeji
CAF ilifuta Uenyaji wa Libya kutokana na Vita inayoendelea Nchini humo ambayo imesababisha kutojengwa kwa Viwanja vilivyoahidiwa kwa ajili ya Fainali hizo zinazoshirikisha Nchi 16
Ghana imesema kuwa ina uhakika wa kupata uenyeji wa michuano hiyo kutokana na miundombinu walizonazo .
Naibu waziri wa michezo nchini Ghana Vincent Oppong Asamoah amesema kuwa nchi iko tayari kuanda AFCON 2017.
Jana Taarifa kutoka nchini Kenya zimedai kuwa Shirikisho la soka nchini humo imewaeleza CAF kuwa wataungana na Tanzania au Uganda au Rwanda kuandaa michuano hiyo.
Ikumbukwe kuwa juzi Tanzania ilitangaza nia ya kuandaa michuano hiyo huku ikidai kuwa itapeleka taarifa kule Cairo,Misri.
Akizungumza na wanahabari juzi jijini Dar es salaama,katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa alisema hatua hiyo inakuja baada ya kamati ya utendaji ya TFF kukutana mapema wikiendi iliyoipita na TFF Itaandaa Maombi hayo na kuyapeleka Serikalini ili kupata baraka za Viongozi wa Nchi kabla kupelekwa huko Cairo Makao Makuu ya CAF.
Mpaka sasa nchi za Tanzania,Ethiopia na Kenya zimeomba kuandaa michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment